Tunaitaka Mamelodi wiki ya Mwananchi - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Apr 2024
Tunaitaka Mamelodi wiki ya Mwananchi - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema amemuomba Rais wa Yanga Injinia Hersi Said kuialika Mamelodi Sundowns katika kilele cha wiki ya Mwananchi baadae mwaka huu

Kamwe amesema Yanga haijamalizana na Mamelodi Sundowns na itapendekeza kama watakuja kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi

"Nimemuomba Rais wa Yanga Injinia Hersi Said kwenye kilele cha wiki ya Wananchi kuufungua msimu wa 2024/25 apambane atuletee Mamelodi Sundowns kwani sisi na wao bado hatujamalizana, " aliandika Kamwe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Wiki ya Wananchi iliyopita Yanga iliialika klabu ya Kaizer Chiefs moja ya klabu kubwa zaidi Afrika ya Kusini

Mamelodi ndio mabingwa wa ligi kuu ya Afrika Kusini kwa misimu sita mfululizo

Kama sio dhurma waliyofanya juzi, Yanga ilikuwa inawatupa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu

Yanga imedhihirisha kuwamudu vijana hao wa Rais wa CAF Patrice Motsepe na wakati wowote Wananchi watakuwa tayari kukabiliana nao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’