Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amesema anajivunia kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga licha ya timu hiyo kushindwa kusonga mbele katika michuano ya ligi ya mabingwa baada ya kupoteza mchezo wa pili wa robo fainali dhidi ya Mamelodi Sundowns kwa mikwaju ya penati
Aziz Ki amesema anajivunia mafanikio ambayo wameyapata katika michuano hiyo licha ya kuwa hawakufikia malengo yao
Amesema walipoishia msimu huu wanaibeba kama changamoto ili kuhakikisha wanarejea wakiwa imara zaidi msimu ujao
Aziz Ki amewataka wachezaji wenzake na mashabiki kutohuzunika, kwani wao ni washindi
"Tukishinda tunasema ALHAMDULILLAH kwa kushindwa pia ni ALHAMDULILLAH maana tumekuja huku tukiwa tumeinua vichwa vyetu juu na tutaondoka tukiwa tumeinua vichwa vyetu juu najivunia kila tunalofanikisha kwa sasa"
"Nawashukuru benchi la ufundi, mameneja na sisi wachezaji tumeonyesha kuwa sisi ni timu na timu kubwa sana timu ambayo ina dhamira ya kurudisha klabu hii katika viwango vya juu kabisa vya Afrika"
"Leo kwa bahati mbaya haikuwa hivyo lakini hatutampa mtu nafasi kutufanya tutilie shaka nguvu ambayo YANGA inayo kama timu na wafuasi kwa mara nyingine tena mlituunga mkono kutoka kila sehemu mliyosafiri kutoka sehemu zote za Tanzania ili tuwepo kwenye mechi hii na nadhani mmeondoka kwa kiburi kwamba wachezaji wenu tunawapa kile mlichostahili
"Kucheza dhidi ya Mamelodi sio kitu rahisi ila kwenye mechi 2 tulionyesha nia yetu ya kufika mbali bila kujali vikwazo tulivyo navyo tutafika kwani sisi ni timu imara na yenye mashabiki wazuri"
"Msimu huu hatujafanikiwa ila tutarudi tukiwa na nguvu zaidi na tutajifunza kutokana na kushindwa kwetu leo"
"Naumizwa na mawazo ya kushindwa kuisaidia timu kufika mbali zaidi ila namshukuru MUNGU siku zote katika nyakati nzuri na mbaya maana yeye pekee ndiye mkuu wa kila kitu na nyie wenzangu mnajua kuwa mimi najivunia nyinyi na kama nilivyosema hatutawahi kuinamisha vichwa vyetu hata tukikutana na timu gani, hatukupoteza ndio, lakini tunatoka na vichwa juu"
"Kwa sababu sisi ni wapambanaji na tunakwenda kufanya kazi ili kufikia malengo yetu msimu ujao, inchalla, nawashukuru watu wote waliofanya safari hii na RAIS wa nchi kwa kujitolea na kutupa hamasa"
"Tunajua zaidi kwamba tulikuja kama shujaa na tutarudi Tanzania kama shujaa lakini tukiwa na mafunzo mengi ya kuleta mchango wetu zaidi katika mwaka ujao"