Licha ya kushindwa kuvuka hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan amewapongeza wachezaji wa Yanga kwa ari na morali yao waliyoonyesha katika mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns
Rais Samia amesema Serikali itaendelea kuiunga mkono Yanga pamoja na kuwapa motisha ili kuhakikisha wanaendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania Kimataifa
Mchezo mzuri Yanga. Mmeonesha kiu na juhudi ya kuiletea heshima nchi yetu hadi kufikia hatua hii. Tunatarajia makubwa zaidi kutoka kwenu kwenye mashindano haya (Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Afrika) msimu ujao. Tutaendelea kuwaunga mkono na kuwapa motisha. pic.twitter.com/QHVFAwcXrt
— Samia Suluhu (@SuluhuSamia) April 5, 2024
ADVERTISE HERE