Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama klabu ya Yanga Simon Patrick amesema licha ya kufahamu hakuna kitakachobadilisha matokeo ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns lakini watumia haki yao kwa kupeleka malalamiko Shirikisho la soka barani Afrika (CAF)
Ni baada ya bao la Yanga kukataliwa katika mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns
Aidha Serikali inaunga mkono uamuzi huo wa Yanga baada ya Naibu Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Mh Hamis Mwinjuma kubainisha kuwa baada ya mazungumzo kati yake na viongozi wa Yanga, wameona ni vyema kulalamika ili kuweka kumbukumbu sawa
Nimetoka kuongea na viongozi wa @YoungAfricansSC na tumekubaliana wanaiandikia CAF kulalamika kuhusiana na goli la wazi lililokataliwa. Haitabatilisha matokeo,lakini angalau tuweke kumbukumbu sawa na ikithibitika hata mwamuzi achukuliwe hatua stahiki. LILE LILIKUWA GOLI HALALI.
β Falsafa Baba! (@MwanaFA) April 5, 2024