Yanga na Tanzania imedhurumiwa - Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Apr 2024
Yanga na Tanzania imedhurumiwa - Gamondi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ameeleza masikitiko yake baada ya Yanga kunyimwa bao halali katika mchezo wa mkondo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundows

Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Loftus huko Afrika Kusini, dakika 90 zilimalizika kwa suluhu ya bila kufungana na Mamelodi kushinda kwa mikwaju ya penati 3-2

Lakini mjadala mkubwa baada ya mechi ni kukataliwa kwa bao alilofunga Aziz Ki ambapo shuti lake la guu la kushoto liligonga mwamba wa juu kisha kudundia ndani

Gamondi amesema ana mashaka na tukio la bao hilo kukataliwa kwani mwamuzi alikuwa na nafasi ya kwenda kujiridhisha kwenye VAR lakini hakufanya hivyo

"Ninachoweza kusema kila mmoja ameona kilichotokea hapa, ukweli ni kuwa Yanga na Tanzania imedhurumiwa wazi wazi"

"Siwalaumu Mamelodi Sundowns, pia nina heshima kubwa kwa nchi ya Afrika Kusini lakini niseme wazi kilichotokea hapa leo ni aibu kwa mpira wa Afrika"

"Nina mashaka na maamuzi ya mchezo huu, pale mchezaji wetu Lomalisa alipopewa kadi ya njano mwamuzi alikwenda katika VAR kujiridhisha kama alistahili kupewa kadi nyekundu"

"Lakini inashangaza kwa nini hakwenda kujiridhisha baada ya bao tulilofunga? Kama tunataka mpira wetu uendelee basi hatupaswi kufanya matukio ya aina hii, ni aibu"

"Timu hii ni mara ya kwanza kufika robob fainali ya mashindano haya, leo hii wamepambana hapa na walistahili kutendewa haki"

"Wananchi zaidi ya Milioni 30 wamdhurumiwa hapa na hili sio jambo zuri," alisema Gamondi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’