Mapema leo, Rais wa Yanga na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vilabu Afrika Eng.Hersi Ally Said alizungumza katika Mkutano na Wanahabari ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Soka Afrika Kusini (South African Football Journalists Association - SAFJA) uliofanyika katika mji wa Sandton, Johannesburg
Wanahabari wa Afrika Kusini walikuwa shauku kubwa ya kumsikiliza Hersi ambaye msimu uliopita aliiongoza Yanga kucheza fainali ya CAF CC huku msimu huu akihakikisha Yanga inavuka hatua ya makundi ya CAF CL sasa ikiwa Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali dhidi ya Mamelodi Sundowns
Miongoni mwa ajenda zilizozungumzwa katika Mkutano huo ni kuihusu Yanga pamoja na Shirikisho la klabu barani Afrika
Hersi ameitaja Yanga kuwa klabu yenye mafanikio zaidi nchini Tanzania huku akibainisha kuwa malengo ya uongozi wake ni kuhakikisha wanaendelea kufanya vizuri katika soka la ndani na Kimataifa
"February 11, Mwaka huu, Yanga ilitimiza miaka 89 tangu kuanzishwa kwake. Ni Klabu kongwe zaidi ya mpira wa miguu Tanzania na ilishiriki kwenye harakati za Uhuru wa Taifa letu. Ni timu ya Wananchi inayogusa maisha ya kila Mtanzania anayependa mpira"
"Yanga ni Klabu yenye mafanikio zaidi Tanzania. Ni Mabingwa mara 29 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, anayefatia amebeba Ubingwa mara 22. Msimu huu mpaka sasa tunaongoza Ligi na tutapambana kuongeza taji la 30 kwenye Kabati letu la makombe"
"Nimshukuru sana Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika, Patrice Motsepe kwa kuanzisha Shirikisho la Vilabu Afrika. Wazo lake ni kupata sauti ya Vilabu ndani ya CAF. Mpira unachezwa na wachezaji na wote wanatoka kwenye vilabu"
"Kuwa na Shirikisho la vilabu inasaidia kufikisha moja kwa moja changamoto zake na kuona jinsi gani mnaweza kusaidia maendeleo ya Vilabu kwa haraka" alisem Hersi
Hii ni mara ya kwanza kiongozi wa timu ya mpira wa miguu Tanzania anapata utambuzi na kuandaliwa Mkutano na Waandishi wa Habari huko Afrika Kusini
Mafanikio ya Yanga pamoja na nafasi yake katika ACA imechangia kupata heshima hiyo