Mshambuliaji Prince Mpumelelo Dube amefungua malalamiko TFF akidai hakusaini mkataba mpya zaidi ya mkataba ambao unaisha mwishoni mwa msimu
Inadaiwa kuwa mshambuliaji huyo ameukana mkataba ambao Azam FC wanasema aliusaini na unaisha mwezi Juni 2026
Mshambuliaji huyo ametinga TFF na mkataba ambao anasema ni halali ambao unafikia ukomo wake mwisho mwa msimu huu yaani Juni 2024
Mshambuliaji huyo amepeleka nyaraka mbalimbali pamoja na vielelezo vingine kuthibishisha kuwa mkataba wake halali unatamatika mwishoni mwa msimu huu
Hivi karibuni Dube aliwaaga Azam kupitia akaunti yake ya Instagram huku akiwashukuru watu mbalimbali katika klabu hiyo kama viongozi wa timu, idara mbalimbali pamoja na mashabiki wa klabu hiyo
Klabu ya Azam Fc imedai bado Dube ni mchezaji wao halali huku ikitangaza kumuweka sokoni ikidai tayari imepokea ofa mbili kutoka klabu za Simba na Al Hilal
Dube tayari amerejesha kila kitu alichokuwa amepewa na Azam Fc anachotaka ni kuvunja mkataba huo uliosalia ili awe mchezaji huru na sio vinginevyo
Sakata hili linafanana kabisa na lile alilowahi kufanya Feisal Salum ambaye mwishoni busara ilitumika baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Samia Suluhu Hassan kuingilia kati na Yanga wakamruhusu Feisal kujiunga na Azam Fc
Pengine Azam Fc nao wanahitaji kutumia busara kwa kumruhusu Dube akajiunge na timu aipendayo na sio kumlazimisha kulipa zaidi ya Tsh Milioni 800 kuvunja mkataba wake
Iwapo kama Dube atashinda madai yake dhidi ya Azam Fc, itakuwa hatua moja zaidi kuelekea kujiunga na timu ya ndoto yake!