Serikali kugharamia safari ya mashabiki Afrika Kusini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Apr 2024
Serikali kugharamia safari ya mashabiki Afrika Kusini

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itagharamia safari ya mashabiki 48 watakaosafiri kwa basi kuelekea Afrika Kusini kuiunga mkono Yanga katika mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa Ijumaa ya wiki hii

Akizungumza mapema leo Makao Makuu ya klabu ya Yanga katika tukio la kuwaaga mashabiki hao, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwaunga mkono huku akitangaza mashabiki waliokuwa wamelipa fedha kwa ajili ya safari hiyo watarudishiwa fedha zao

"Tunafahamu Klabu yetu ya Young Africans SC ina mchezo mwingine wa pili kule Afrika Kusini hivyo Uongozi wenu umefanya jitihada za kupeleka Ombi katika Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo chini ya Waziri wetu Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro la kusafirisha mashabiki kwa njia ya Basi na tunaishukuru Wizara kwa kukubali Ombi letu"

"Wizara itahudumia gharama zote za safari ya kuelekea Afrika kusini yenye Wanachama na Mashabiki wetu 48 kuanzia Nauli mpaka pesa ya kujikimu, hivyo sisi Young Africans tunaishukuru sana Wizara"

"Hapo mwanzo tulitangaza watu watakaosafiri walipaswa kuwa na shilingi laki 6 na tulipata watu 30, niwahakikishie baada ya Wizara kukubali kusafirisha Wanachama na Mashabiki wetu,zile laki 6 zitarudishwa kwa wenyewe"

"Niwatakie safari njema na nina imani safari yetu ya kurudi itakuwa nzuri kwakuwa tutarudi tukiwa tayari tumeshafuzu hatua ya nusu Fainali," alisema Hersi

Nae Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Hamis Mwinjuma amewataka mashabiki na wanachama waliopata nafasi ya kusafiri na timu kuhakikisha wanakwenda kuiongezea hamasa Yanga ili kupata matokeo mazuri yatakayowapa nafasi ya kutinga nusu fainali ya ligi ya mabingwa

"Kwanza niwapongeze sana kwa uamuzi wa kusafiri kwa basi kwani mngeweza kusema mbaki nyumbani na kutazama mechi kwenye Tv, Hii inamaanisha nyinyi ni wafia Yanga, Hongereni sana"

"Uzuri kiwango cha timu yetu mmekiona na kinaridhisha, mpinzani tunayekwenda kucheza naye hana faida ya Mashabiki wengi hivyo naamini Nguvu ya kushangilia ambayo mnayo itakwenda kuleta tija kwenye mchezo wetu siku ya ijumaa"

"Nimekuja hapa kufikisha salamu za Serikali chini ya Daktari Samia Suluhu Hassan, kila kinachoendelea yeye anafuatilia kwa umakini na anawatakia kila la heri kwenye Safari hii na kwenye mchezo wetu siku ya ijumaa," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’