Huyu sasa ndio Mkude

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Mar 2024
Huyu sasa ndio Mkude

Achana na kazi kubwa iliyofanywa na mwenye mechi yake, Mudathir Yahya Abas, Mamelodi Sundowns hawakufua dafu eneo la kiungo kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Jonas Mkude

Unaweza kusema mechi dhidi ya Mamelodi jana ndio mechi bora zaidi ambayo Mkude amecheza tangu aliposajiliwa na Yanga akitokea Simba

Huyu ndio Mkude ambaye amedumu kwenye soka la Tanzania kwa muda mrefu na kama ataendeleza hiki alichofanya katika mchezo dhidi ya Mamelodi, ni wazi kocha Miguel Gamondi hatakuwa na sababu ya kutompa nafasi katika mechi nyingine

Kukosekana kwa Khalid Aucho kulizua hofu kubwa kwa Wananchi kabla ya mchezo lakini baada ya dakika 90 hakuna aliyelalamika baada ya kumshuhudia Mkude akiwa katika kiwango bora kabisa

Matokeo haya ya suluhu ni faida kwa Yanga kuliko Mamelodi kwani yataongeza ari ya timu kuelekea mchezo wa marudiano utakaopigwa Ijumaa huko Afrika Kusini

Mtazamo wa wengi waliamini Yanga ingepoteza mchezo huo hasa kwa aina ya kikosi walichotumia

Lakini pia katika mchezo wa marudiano presha itakuwa upande wa Mamelodi kwa sababu kama Yanga itafunga bao ugenini maana yake Mamelodi watalazimika kufunga mabao mawili na idadi itaongezeka kwa kila bao ambalo Yanga watafunga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’