Nahodha wa Yanga Nadir Haroub amesema baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolaitta Dicha nyumbani leo, watahamasishana kuhakikisha wanapata matokeo kwenye mchezo wa ugenini ili kuweza kutinga hatua ya makundi.
Nadir amesema licha ya kukosa nafasi nyingi, ushindi wa mabao 2-0 uliopatikana nyumbani sio matokeo mabaya.
"Ushindi tuliopata nyumbani sio matokeo mabaya. Tunajua mchezo wa marudiano nchini Ethiopia utakuwa mgumu. Lakini Yanga tuna kawaida ya kuhamasishana sana tunapocheza ugenini," amesema.
"Tutahakikisha tunapata matokeo yatakayotuwezesha kutinga hatua ya makundi huko huko ugenini."
Yanga inahitaji sare au kufungwa sio zaidi ya mabao mawili kwenye mchezo wa marudiano ili iweze kufuzu hatua ya makundi.

ADVERTISE HERE