Pale wachambuzi wanapoukosea mpira wa miguu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Mar 2024
Pale wachambuzi wanapoukosea mpira wa miguu

Huko Afrika Kusini mchezo wa ligi ya mabingwa kati ya Yanga dhidi ya Mamelodi Sundowns unachukuliwa kimtizamo tofauti kabisa na jinsi ilivyo hapa nchini

Imekuwa bahati mbaya asilimia 90 za uchambuzi unaofanywa katika vyombo vya habari hapa nchini ni wa kuwakatisha tamaa mashabiki wa Yanga wakiaminishwa kuwa Mamelodi ni bora sana na kuwa Yanga haina uwezo wa kushinda dhidi yao

Imefika hatua 'inaboa' kusikiliza vipindi vya michezo kwani zaidi utasikia majina ya wachezaji wa Sundowns yakitajwa kipindi kizima kana kwamba Yanga haina wachezaji bora ambao wanastahili kufanyiwa uchambuzi

Uzuri mpira unachezwa hadharani na takwimu wakati mwingine zinaweza kuzungumza kwa uhalisia zaidi kuliko maoni binafsi

Wachambuzi wengi wanatoa maoni binafsi tu ambayo wakati mwingine sio uhalisia wa kile kinachotokea uwanjani ndani ya dakika 90

Ni tofauti na uchambuzi unaofanywa na media za Afrika Kusini wao wamejikita zaidi katika takwimu na kuzungumza mpira jambo linalowafanya waamini mchezo dhidi ya Yanga hautakuwa mwepesi

Ni wazi mechi itakuwa ngumu lakini sio sahihi kusema Yanga haina nafasi ya kushinda mchezo huo eti kwa kuwa inacheza dhidi ya timu yenye kikosi ghali zaidi

Mechi itakutanisha wachezaji 11 dhidi ya 11 na kila timu ina nafasi ya kucheza katika uwanja wake wa nyumbani

Yanga imejipanga na imedhamiria kushinda mchezo wa kwanza utakaopigwa dimba la Mkapa Jumamosi, INAWEZEKANA

Wale ambao hawakujifunza na kile walichofanya Yanga katika michuano ya kombe la Shirikisho msimu uliopita, basi wajiandae na aibu nyingine kubwa pale itakapotokea Yanga imetinga nusu fainali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’