Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kimehitimisha ushiriki wa michuano maalum ya FIFA Series 2024 huko Azerbaijan kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mongolia
Mabao ya Stars yalifungwa na Kelvin John, Abdul Suleiman na Novatus Dismus
Ulikuwa mchezo ambao Stars iliwakalia kooni Wamongolia kwa muda wote wa mchezo pengine wangeweza kufunga mabao mengi zaidi
Huo ulikuwa mchezo wa pili baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Bulgaria
ADVERTISE HERE