Mudathir kuibeba Yanga dhidi ya Mamelodi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Mar 2024
Mudathir kuibeba Yanga dhidi ya Mamelodi

Kiungo wa Yanga Mudathir Yahya amepewa jukumu la kubeba hamasa ya mchezo wa mkondo wa kwanza ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa Jumamosi, March 30 katika uwwnja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema Jumamosi ni Muda Day simu ziite, tukutane kwa Mkapa!

"Kazi tuliyonayo sasa hivi ni kuwapigia simu watu wote tukutane kwa Mkapa. Tutawapigia simu watu wote wanaotaka na wasiotaka"

"Kama uko ofisini kuna simu ya ofisi itumie, piga kwa nmtu yoyote mwambie wewe unahitajika kwa Mkapa"

"Pigia simu mtu yoyote awe shabiki wa Yanga, awe shabiki wa Azam, awe shabiki wa Mtibwa au timu yoyote, mpigie simu waambieni wanahitajika kwa Mkapa"

"Jumamosi ni siku yetu Wananchi, tutakwenda kumuonyesha Mamelodi kuna pande anaweza kutamba lakini sio pande ambazo sisi Yanga tumo"

"Ni uwanja wetu, ni ardhi yetu na timu yetu, tutakwenda kutamba sisi katika uwanja wa Benjamin Mkapa"

"Nawakaribisha Wanayanga mapema kabisa mje uwanja wa Benjamin Mkapa, mimi nitakuwa mtu wa kwanza kuingia uwanjani mapema baada ya mageti kufunguliwa. Njooni mapema tujadiliane kabla ya mechi"

"Utaratibu wa futari kwa wale walio katika mfungo umeandaliwa, njooni mapema, kutakuwa na burudani nyingi za kuwfanya mfurahi kabla ya mchezo," alitamba Kamwe

Kamwe amesema uzinduzi wa hamasa kuelekea mchezo huo utafanyika kesho Jumanne Kariakoo. Jumatano hamasa itafanyika Makumbusho na Alhamisi hamasa itahitimishwa Tandika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
37m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’