FT : Yanga 2-0 Wolaitta Dicha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Apr 2018
FT : Yanga 2-0 Wolaitta Dicha
Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wamejiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kuichapa Wolaitta Dicha ya Ethiopia kwa mabao 2-0 kwenye mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa.

Yanga ilianza kuhesabu bao la kuongoza mapema tu kwenye sekunde ya 38 baada ya krosi ya Haji Mwinyi kutoka upande wa kushoto kutua kichwani kwa Raphael Daudi Lothi na kuiandikia Yanga bao la kuongoza.

Licha ya Dicha kutawala mchezo huo kwa muda mrefu, Yanga ndio iliyokuwa hatari zaidi kupitia mashambulizi ya kushitukiza.



Kwenye dakika ya saba nusura Lothi aiandikie Yanga bao la pili kama si shuti lake akiwa ndani ya 18 kupaa juu ya lango.

Majaribio mengine yalifanywa na Emanuel Martin, Yusuph Mhilu na Ibrahim Ajib lakini yaliweza kuzuiwa na mlinda lango wa Dicha huku mpira wa Ajib ukitoka nje sentimeta chache.

Kipindi cha pili Yanga ilirejea kwa kasi ikitumia mfumo ule ule wa mashambulizi ya kushitukiza na iliandika bao la pili kwenye dakika ya 54 mfungaji akiwa Emanuel Martin aliyeunganisha vyema krosi ya Yusuph Mhilu.

Dicha walitengeneza nafasi kadhaa kwenye kipindi cha pili lakini uimara wa mlinda lango Youthe Rostand uliiwezesha Yanga kuondoka na ushindi bila kuruhusu bao.



Safu ya ulinzi ya Yanga iliyokuwa chini ya Andrew Vicent na Abdallah Shaibu 'Ninja' wakisaidiana na walinzi wa pembeni Haji Mwinyi na Hassani Kessy pamoja na viungo Kamusoko na Buswita waliweza kuondoa hatari zote zilizoelekezwa langoni na Dicha iliyokuwa ikisaka angalau bao la ugenini.

Chikupe alishindwa kumaliza mchezo huo baada ya kuumia kwenye dakika ya 74 na nafasi yake kuchukuliwa na mkongwe, Nadir Haroub Cannavaro huku Kamusoko naye akitolewa nafasi yake kuingia Patto Ngonyani.

Juma Mahadhi aliingia kuchukua nafasi ya Lothi kwenye dakika za lala salama

Yanga ingeweza kufunga mabao zaidi kama Ajib na Mhilu wangezitumia vyema nafasi walizopata kwenye kipindi cha pili.

Matokeo hayo yanaiweka Yanga katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi kwani kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa siku 10 zijazo nchini Ethipoia, Yanga inahitaji kuizuia Dicha isifunge zaidi ya mabao mawili.

Habari njema zaidi kwa Yanga kwenye mchezo huo wachezaji wake wanne, Obrey Chirwa, Papi Tshishimbi, Said Juma Makapu na Kelvin Yondani watarejea kikosini baada ya kuwa wamemaliza kutumikia adhabu zao za kukosa mchezo mmoja.



Idadi kubwa ya mashabiki wa Yanga wamejitokeza kwenye uwanja wa Taifa kushuhudia mtanange huo tofauti na ilivyokuwa kwenye mchezo dhidi ya Township Rollers.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’