Wachezaji watatu wa Yanga kati ya watano waliokuwa na timu ya Taifa ya Tanzania huko Azerbaijan wameondoka kurejea nchini kuungana na wenzao wanaojiandaa na mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns
Mudathir Yahya, Ibrahim Bacca na Clement Mzize wameondoka Azerbaijan huku Bakari Mwamnyeto na Aboutwalib Mshery wakiendelea kubaki kusubiri mchezo dhidi ya Mongolia utakaopigwa Jumatatu
Pamoja na Mwamnyeto na Mshery, wachezaji wengine watakaoendelea kukosekana kutokana na majukumu ya timu za Taifa ni Djigui Diarra, Stephane Aziz Ki, Kennedy Musonda na Pacome Zouzoua
ADVERTISE HERE