Kwa Yanga hii hawataamini macho yao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Mar 2024
Kwa Yanga hii hawataamini macho yao

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki na wanachama wa timu hiyo kutoyumbishwa na baadhi ya wachambuzi wa soka nchini kwani wana timu nzuri

Kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi utakaopigwa Jumamosi ya March 30, Kamwe amesema Yanga itakwenda kuwafunga midomo wale wote wenye mashaka nao kwa kuibuka na ushindi dhidi ya Mamelodi katika uwanja wa Benjamin Mkapa

"Najua wachambuzi wengi na waandishi hawaipi nafasi Yanga dhidi ya Mamelodi. Lakini ni ukweli sisi tuna timu nzuri kuliko Mamelodi"

"Nina uhakika Wachezaji sita mpaka saba wanaweza kuanza kwenye kikosi cha Mamelodi. Tunaichukulia poa Yanga kwa sababu tu inatokea Tanzania. Lakini hii Klabu ingekuwa ipo DR Congo ingesifiwa sana kuliko inavyosifiwa sasa"

"Mwananchi usisikilize uchambuzi wa mchambuzi yoyote yule. Tusipotezwe kwenye dira yetu. Yanga ikiamua jambo lake hatuwezi kufeli. Nina uhakika kwa zaidi ya asilimia 100 kuwa tunakwenda kushinda mchezo ujao. Mtu akikwambia Mamelodi ina wachezaji wazuri mwambie hata sisi tuna wachezaji bora kuliko wao," alisema Kamwe

Msimu uliopita wakati Yanga inashiriki CAF CC, ilikumbana na mazingira kama haya lakini pasipo matarajio ya wengi ilifanikiwa kucheza fainali ya michuano hiyo na kukosa taji kikanuni baada ya matokeo ya sare ya 2-2 dhidi ya USM Alger

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’