Klabu ya Yanga imewapa fursa Wananchi wote kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi March 30 katika mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema uongozi umezingatia changamoto mbalimbali ambazo Wananchi wanaweza kukutana nazo katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu pamoja na muda wa mchezo huo kupigwa saa 3 usiku
"Uongozi pia unafahamu kuwa Jumamosi itakuwa mkesha wa kuelekea sikukuu ya Pasaka hivyo tumetoa ahueni kwa Wananchi kwa kuondoa kiingilio katika Mzunguuko"
Kamwe pia ametangaza viingilio vya madaraja mengine; VIP A - 30,000/- VIP B - 20,000/- VIP C - 10,000/-
Haya Wananchi mshindwe wenyewe kuja uwanjani, Mzunguuko ni BURE
Yanga pia imetangaza mkakati wa kusafiri na mashabiki Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaopigwa April 05
"Uongozi wa Klabu umekubaliana kuweka mkakati wa kupeleka mashabiki Afrika Kusini kwenye mchezo wa marudiano. Kama tulivyofanya wakati wa mchezo wetu wa nusu fainali CAFCC dhidi ya Marumo"
"Twenzetu kwa Madiba (kwao kama kwetu) season 2 inaanza na Bei ya kushiriki ni ile ile tshs 2000 tu. Vile vile tumeaanda usafiri wa kwenda Afrika Kusini kwa njia ya basi, ambapo utahitaji kuwa na kiasi cha Tsh 600,000 gharama za kwenda na kurudi"
"Watu 10 kutoka Morogoro tayari wameshalipa, endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii tutaweka utaratibu wa namna ya kulipia, " alisema Kamwe