Yao hatihati kuikabili Mamelodi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Mar 2024
Yao hatihati kuikabili Mamelodi

Mlinzi wa kulia wa Yanga Yao Kouassi alichanika nyama za paja katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc, nafasi yake ya kucheza mechi ya ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns ni 50/50

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Msemaji wa Yanga Ali Kamwe, alibainisha kuwa taarifa ya kitatibu iliyotolewa na daktari wa Yanga Moses Itutu imethibitisha majeraha hayo na tayari ameshaanza matibabu

"Yao Kouassi alichanika nyama za paja kwa mujibu wa taarifa ya daktari wetu wa timu, tayari ameshaanza matibabu, madaktari wanapambana kuona kama ataweza kutumika katika mchezo dhidi ya Mamelodi lakini nafasi yake ni 50/50," alisema Kamwe

Kamwe pia alibainisha hali za majeruhi wengine ambapo amesema Kibwana Shomari hali yake imeimarika na siku ya Jumatatu ataanza mazoezi ya uwanjani kama ilivyo kwa Zawadi Mauya ambaye yuko tayari kuanza mazoezi

Kuhusu hali ya Khalid Aucho, Kamwe amesema kiungo huyo anakamilisha awanu ya pili ya program maalum ambayo ni mazoezi ya Gym. Akimaliza program hiyo nae ataanza mazoezi ya kucheza mpira uwanjani

Pia aligusia kuhusu Pacome Zouzoua ambaye pia alipata shida ya goti katika mchezo dhidi ya Azam Fc

Baada ya mchezaji huyo kuitwa timu ya Taifa ya Ivory Coast, Kamwe amesema Yanga inasubiri taarifa ya madaktari wa timu ya Taifa baada ya mchezaji huyo kuhitajika kuitumikia Ivory Coast kwenye mechi mbili za Kimataifa za kirafiki dhidi ya Benin na Uruguay

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
23h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’