Wakati klabu ya Yanga leo ikitarajiwa kutoa taarifa juu ya majeraha waliyopata wachezaji Pacome Zouzoua na Yao Kouassi katika mchezo uliopita ligi kuu dhidi ya Azam Fc, Meneja wa Habari na Mawasiliano Ali Kamwe amewataka mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na hofu kwani ni wao wenye nafasi ya kuamua matokeo ya mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns
Jumamosi March 30 Yanga itakuwa mwenyeji wa Mamelodi katika mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika
"Niwaambie mashabiki wa Yanga, sisi tuna nafasi ya kuisaidia timu yetu kupata ushindi katika mchezo dhidi ya Mamelodi. Kama tukiamua, tunaweza kuimaliza mechi hii ya robo fainali hapa Dar"
"Sisi Yanga tukiwa wamoja na kunuia kushinda mchezo huu, nawahakikishia tunakwenda kupata ushindi. Tunao uwezo wa kumfunga Mamelodi Sundowns"
"Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuelekea mchezo huo, twendeni pamoja kama Yanga, twendani tukaionyeshe Afrika na Dunia kwa nini slogan wetu ni Daima Mbele, Nyuma Mwiko"
"Hakuna cha kuhofia wala hakuna wasiwasi, tunakwenda kuikabili Mamelodi March 30 kana kwamba hakuna mchezo mwingine wa marudiano"
"Mchezo huu tutaingia tukiwa Yanga kamili, Yanga yenye hamasa kubwa kutoka kwa mashabiki na wanachama wetu kwenda kucheza mchezo huu mkubwa," alisema