Bado mashabiki wa Yanga hawana uhakika na hatma ya kiungo wao Khalid Aucho kuelekea mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa March 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa goti uliotarajiwa kumuweka nje kwa wiki tatu, Aucho amepambana kujiimarisha na dalili ni njema huenda akauwahi mchezo huo
Daktari wa Yanga Moses Etutu amesema Aucho amekuwa na maendeleo mazuri baada ya matibabu yake na wiki hii ataanza mazoezi mepesi ya uwanjani
"Baada ya kufanyiwa upasuaji kuna program maalum tulimpatia ili kuharakisha uponaji wake. Tunafurahi yeye mwenyewe (Aucho) anajituma"
"Amemaliza awamu ya kwanza ya program yake, wiki hii tunatarajia ataanza mazoezi mepesi ya uwanjani kabla ya kujumuika na wenzake kuendelea na program za timu," alisema
Ni siku 12 zilizosalia kuelekea mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns, uwepo wa Aucho ktika mchezo huo itakuwa habari nzuri zaidi kwa Wananchi