Maneno aliyosema Tshishimbi baada ya kutua Dar

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
24 Jul 2017
Maneno aliyosema Tshishimbi baada ya kutua Dar
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika ndiye aliyefanikiwa kumleta Tanzania kiungo wa Mbabane Swallows Papi Kabamba Tshishimbi juzi.

Baada ya kutua mikononi mwa Yanga, Tshishimbi amesema kuwa anajisikia faraja na anaamini hatafanya kosa kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria wa soka la Tanzania.

"Nafurahi kuja Yanga, ni sehemu ambayo itanipa changamoto mpya. Nilisikia kocha wao alikuja kunitazama na kuridhishwa na uwezo wangu, sina budi kuonyesha zaidi hapa," alisema kiungo huyo.

"Kwa kuwa walionyesha nia ya dhati ya kunisajili, nami nipo tayari kufanya kazi. Nafikiri tutakuwa na makubaliano mazuri katika kusaini hapa," alisema.

Aidha Nyika amesisitiza kuwa Yanga imedhamiria kusuka kikosi imara kitakachofanya vyema hasa kwenye michuano ya Kiamtaifa na Kamati yake ya usajili imesajili wachezaji kwa kufuata misingi hiyo.

"Nafikiri nimekuwa nikisema mara kwa mara, kamati yangu imedhamiria kukisuka kikosi chetu kwa umakini mkubwa, tukiyafanyia kazi mapendekezo ya makocha wetu na si kukurupuka kama wanavyofanya wengine," alisema.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’