Yanga imekusanya alama nyingine tatu uwanja wa Azam Complex baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Bao pekee la Stephane Aziz Ki limetosha kuihakikishia Yanga ushindi muhimu ambao umewafanya waongeze gap la pointi kileleni kuwa nane
Ilikuwa mechi ambayo pengine Yanga ilihitaji alama tatu zaidi kuliko kutandaza soka la burudani ambalo Wananchi wamezoea kuliona
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema ratiba imekuwa changamoto vijana wake wana fartique kutokana na kucheza mechi mfululizo
Gamondi amesema vijana wake watahitaji mapumziko kabla ya mchezo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili, March 17
ADVERTISE HERE