Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Taifa kuipa sapoti timu ya Yanga itakapokuwa inamenyana na Welayta Dicha ya Rthiopia kesho.
Ten amesema wingi wa mashabiki uwanjani utaongeza hamasa kwa wachezaji na kuiwezesha Yanga kuibuka na ushindi muhimu nyumbani.
"Tuje kwa wingi uwanja wa Taifa, tuje tumevaa jezi za njano ili tuupendezeshe uwanja," amesema Ten.
"Mashabiki ni wachezaji wa 12, uwingi wetu uwanjani utaongeza kitu kwa wachezaji. Mchezo huu ni lazima tushinde kama tunataka kusonga mbele."
Viingilio vya mchezo huo VIP A ni Tsh 15,000/- VIP B na C ni Tsh 10,000/- wakati mzunguuko itakuwa Tsh 3,000/- tu.
Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa kumi kamili jioni.

ADVERTISE HERE