Kiungo wa Yanga Khalid Aucho tayari ameanza mazoezi mepesi baada ya upasuaji mdogo wa goti aliofanyiwa hivi karibuni
Hii ni habari njema kwa mashabiki wa Yanga kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa katika kipindi cha siku 16 zijazo
Aucho alitarajiwa kukaa nje kwa wiki tatu, matumaini ni makubwa anaweza kuwahi mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu
Yanga itakuwa na dakika 180 za kuisaka tiketi ya kutinga nusu fainali CAF CL mbele ya moja ya timu bora barani Afrika kwa sasa, Mamelodi Sundowns
ADVERTISE HERE