Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa kati ya Yanga dhidi ya Mamelodi Sundowns utakuwa na ushindani na watakuwa tayari kukabiliana na mabingwa hao wa Afrika Kusini
Akizungumza baada ya droo ya robo fainali iliyofanyika nchini Misri jana, Gamondi alisema anaifahamu vyema Mamelodi Sundowns kwani ni miongoni mwa klabu alizowahi kuzifundisha
"Nawafahamu vyema Mamelodi Sundowns, wanacheza soka linalofanana na sisi, nimewahi kuifundisha timu hii na kupata mafanikio hivyo sio wageni kwangu"
"Mamelodi kwa sasa ni miongoni mwa timu kubwa barani Afrika, ukiangalia bajeti yao ya usajili utabaini hilo. Waliwahi kumnunua mchezaji Argentina kwa dola milioni 4. Hivyo hii ni timu kubwa ukilinganisha na sisi"
"Lakini tunapofika uwanjani ni wachezaji 11 dhidi ya 11, nawaamini wachezaji wangu tunaweza kuwashangaza katika hatua hii"
"Tunataka Yanga iwe miongoni mwa timu tano bora barani Afrika, sasa hatuwezi kufika hapo pasipo kuchuana na hawa ambao tayari wako juu, "alisema Gamondi
Nae Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema uongozi wake umepokea droo hiyo ya robo fainali na watajiandaa, kuhakikisha wanafanya vizuri lengo likiwa kuivusha Yanga nusu fainali