Ihefu Fc ni timu ya nane kufungwa mabao matano na Yanga katika mashindano yote msimu huu ikiwa timu ya nne kuchezea 5G katika ligi kuu ya NBC
Wananchi walinza 5G kwa KMC, wakafuata JKT Tanzania, Simba nao walikumbana na adhabu
Ndio! Ni hao hao Simba ambao huko mitandaoni mashabiki wao wanaumia 5G waliyozawadiwa Ihefu Fc. Msemaji wa Yanga Ali Kamwe amesema huo ni wivu tu!
Nafikiri baadhi ya wachambuzi hawapaswi kupoteza muda mwingi kuzungumzia masuala ambayo hayapo, walipaswa kumpongeza kocha Miguel Gamondi na benchi lake la ufundi, wachezaji, viongozi na hata mashabiki wa Yanga ambao muda wote wapo uwanjani kuhamasisha wachezaji wao
Kuna kazi kubwa imefanyika kuifikisha Yanga hapa ilipo na haikuwa kazi ya siku moja
Sio kwa ndani tu, Kimataifa Yanga ni miongoni mwa timu nne zilizofanya vizuri zaidi katika kipindi cha misimu miwili
Utazungumzia Al Ahly (mabingwa waliopita CAF CL), Mamelodi (Mabingwa AFL), USM Alger (Mabingwa CAF CC na Super Cup) na Yanga iliyocheza fainali CAF CC msimu uliopita na msimu huu imetinga robo fainali CAF CL
Mwishoni mwa msimu wa 2021/22 Yanga ilikuwa nafasi ya 75 katika ranking za CAF lakini ndani ya miaka miwli Yanga imechupa mpaka nafasi ya 12 ikikusanya alama 31
Hivi unapata wapi jeuri ya kuhoji matokeo ya vipigo wanavyotoa katika ligi ya ndani? Ina maana Yanga ina pesa nyingi sana za kuhonga kila timu ndani na nje?
Nafikiri sehemu pekee ya kushindana na Yanga ni uwanjani kama kuna timu inadhani iko bora sana basi waombe hata mechi ya kirafiki na Wananchi na uwanja wachague wenyewe!
Hizi propaganda zinazoenezwa ni dalili za baadhi ya timu kushindwa na sasa 'wanatupa taulo' kwa njia hiyo