Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema hawana hofu yoyote kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa kesho Ijumaa huko Misri
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Gamondi amesema wanatambua wanakwenda kuchuana na timu bora zaidi barani Afrika lakini hawahofii na malengo yao ni kushinda mchezo huo
"Tuko hapa kushindana, vijana wangu wako tayari na tumedhamiria kushinda mchezo dhidi ya Al Ahly"
"Tunajua hautakuwa mchezo rahisi kwa sababu tunacheza na timu bora zaidi barani Afrika lakini hatuna hofu yoyote, tunakwenda kutimiza kile tulichofanya katika kiwanja cha mazoezi ili kutafuta ushindi"
"Takwimu zetu katika michuano hii ziko wazi, tunajua utakuwa mchezo wa mbinu zaidi nasi tumejipanga vizuri"
"Nimekuwa katika soka la Afrika kwa takribani miaka 25, hivyo niwaambie tu, hatujaja hapa kutembea. Tumekuja kuonyesha uwezo wetu na muhimu kuwapa furaha mashabiki wetu," alisema Gamondi
Mchezo dhidi ya Al Ahly utapigwa kesho Ijumaa, saa 1 usiku katika uwanja wa Kimataifa wa Cairo