Hivi karibuni mshambuliaji wa zamani wa Yanga Fiston Mayele aliingia katika mgogoro na waliokuwa waajiri wake hao baada ya kutoa tuhuma nzito kwa mashabiki na baadhi ya viongozi wa timu hiyo
Kauli yake ya kudai kutukanwa na kutupiwa majini na anaodai kuwa ni watu wa Yanga sio tu iliwakera Wananchi, pia iliikosea heshima Yanga ambayo ndio sababu ya yeye kupata nafasi ya kuonekana na kusajiliwa Pyramids Fc
Kilichotokea kwenye mechi zilizopita za ligi ya mabingwa, ni somo kwa Mayele kuwa ubora na umaarufu wake haukusababishwa na uwezo wake pekee, bali hamasa na mapenzi aliyopewa na wananchi vilichangia yeye kufanya vizuri
Pyramids imeondoshwa katika ligi mabingwa mapema tu baada ya kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa TP Mazembe juzi
Mayele alikuwa sehemu ya kikosi kilichoanza mchezo huo lakini hakupata hata shoot on target!
Katika mechi nne alizocheza michuano ya CAF msimu huu akiwa Pyramids, Mayele ametoa assist moja tu na hana bao lolote
Huku alikotoka Yanga mambo yanazidi 'kunoga' baada ya Wananchi kutinga robo fainali kibabe kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CR Belouizdad
Mshambuliaji Joseph Guede aliyetua dirisha dogo tayari amefunga akaunti ya mabao akifunga bao moja katika mchezo dhidi ya CR Belouizdad
Kennedy Musonda aliyekuwa nae katika kikosi msimu uliopita ana mabao mawili sawa na kiraka Mudathir Yahya. Pacome Zouzoua taratibu anachukua ufalme akiwa na mabao matatu
Huu ni ujumbe kwa Mayele kuwa ukubwa ambao alidhani anao ulitokana na nguvu ya Wananchi na sasa ukubwa huo hanao kwa sababu ile sapoti aliyokuwa akiipata akiwa Yanga haipo tena