CAF wajichanganya kadi za Yondani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Apr 2018
CAF wajichanganya kadi za Yondani
Uongozi wa Yanga umesema kwa mujibu wa takwimu zilizopo, mlinzi Kelvin Yondani hakuonyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa kati ya Yanga dhidi ya Township Rollers uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Yondani ni miongoni mwa wachezaji wanne waliozuiwa na CAF kucheza mchezo wa kwanza wa mtoano kombe la shirikisho kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi.

Kulingana na takwimu zilizopo, Yondani alionyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo wa marudiano nchini Botswana lakini ni Pato Ngonyani aliyeonyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo wa kwanza.

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema tayari wamewasilisha malalamiko yao CAF na huenda majibu yakatolewa mapema kabla ya mchezo keshokutwa.

Makosa kama hayo pia yanamuhusu kocha msaidizi Noel Mwandila ambaye amezuiwa kushiriki mchezo huo kimakosa wakati aliyestahili adhabu hiyo ni Shedrack Nsajigwa.

Nsajigwa alitolewa kwenye benchi la Yanga na mwamuzi wa mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa kati Township Rollers dhidi ya Yanga nchini Botswana.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’