Yanga vs CRB; Mwananchi tayari umekata tiketi?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Feb 2024
Yanga vs CRB; Mwananchi tayari umekata tiketi?

CR Belouizdad walitua jana na mkwara mzito wakija na kundi kubwa la mashabiki kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumamosi Februari 24 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Msafara wa Belouizdad umeongozwa na Rais wa klabu hiyo ambapo pia Kocha Mkuu wa Stars Adel Amrouche ambaye ni raia wa Algeria ameonekana akiwa bega kwa bega na timu hiyo

Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani CR Belouizdad wanazitaka alama tatu za mchezo huo, lakini hawawezi kuzipata kama Wananchi tutakwenda kujaza dimba la Mkapa na kuhakikisha tunawahamasisha wachezaji wetu kwa dakika zote 90 za mchezo

Ni mechi ambayo ushindi unaweza kutosha kuipelekea Yanga robo fainali hii ikitegemea na matokeo ya mchezo kati ya Medeama dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa kesho Ijumaa

Jambo la msingi kwa Yanga ni kushinda mchezo huo pasipo kujali matokeo ya mechi nyingine kwani bado safari ya robo fainali iko mikononi

Ni siku mbili tu zilizosalia kukata tiketi, hii ni mechi ambayo Belouizdad watapaswa kufungwa nje na ndani ya uwanja

Hii ni mechi ya kisasi, Belouizdad wanapaswa kufahamu kwa nini Yanga ni mabingwa wa kihistoria Tanzania....!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’