Kocha Mkuu wa timu ya taifa Tanzania 'Taifa Stars' Adel Amrouche ni sehemu ya msafara wa kikosi cha timu ya CR Belouizdad uliokuja nchini kwa ajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumamosi
Kocha huyo alionekana kuwa karibu na kikosi hicho kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa (Mw. Nyerere International Airpot) hadi katika kambi ya kikosi hicho katika moja ya Hotel za Kitalii, Jijini Dar es Salaam
Amrouche alifungiwa mechi nane na CAF baada ya kutoa kauli zenye utata katika michuano ya Afcon 2023 iliyomlizika hivi karibuni huko Ivory Coast
Msafara wa Belouizdad umejumuisha idadi kubwa ya mashabiki ambao walinza kuwasili nchini tangu jana
ADVERTISE HERE