Lwandamina 'akuna kichwa' safu ya ulinzi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Apr 2018
Lwandamina 'akuna kichwa' safu ya ulinzi Yanga
Kukosekana kwa Kelvin Yondani na Said Juma 'Makapu' katika kikosi cha Yanga kwenye mchezo wa keshokutwa dhidi ya Welayta Dicha kunamlazimu kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina kuiuanda upya safu yake ya ulinzi.

Lwandamina atalazimika kumtumia nahodha Nadir Haroub au beki chipukizi Abdallah Shaibu ambaye hajacheza mchezo wowote tangu alipoumia kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi mwezi Januari 2018.

Muhimili wa safu ya ulinzi ya Yanga utamtegemea zaidi beki kisiki Andrew Vicent Chikupe.

Lakini pia kiungo Pato Ngonyani ana uwezo wa kucheza nafasi ya ulinzi na haitakuwa mara ya kwanza kwa kiungo huyo mkabaji kucheza beki.

Wakati Yanga ikinolewa na Hans van Pluijm, mara nyingi alikuwa akimtumia Pato kama mlinzi wa kati kuwasaidia Yondani, Nadir na Bossou.

Lwandamina anaweza pia akatumia walinzi watatu nyuma ili kumarisha zaidi safu ya ulinzi.

Anaweza kumtumia Nadir kama mlinzi wa mwisho wakati Chikupe na Shaibu/Pato wakicheza pembezoni mwake.

Aina ya uchezaji wa Chikupe na Shaibu hauwafanyi kuwa walinzi wazuri wa mwisho wanahitaji uwepo wa mkongwe kama Cannavaro kuweza kuwapanga.

Yondani amekuwa akiifanya kazi hiyo kikamilifu anapocheza na Chikupe.

Ukiondoa hofu iliyopo kwenye safu ya ulinzi, kikosi cha Yanga kina wachezaji wengi wanaoweza kucheza nafasi zilizosalia.

Chipukizi Maka Edward, Thabani Kamusoko na Pius Buswita hawa wanaweza kutuliza kabisa nafasi za Makapu na Tshishimbi wakati kwenye ushambuliaji upo uwezekano mkubwa kwa Donald Ngoma kurejea kikosini kuchukua nafasi ya Obrey Chirwa.

Pia Yanga inao washambuliaji wengine kama Yohana Nkomola, Juma Mahadhi na Amissi Tambwe ambaye naye huenda akawa tayari kucheza mchezo huo.

Yanga iliweka kambi mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa, keshokutwa Jumamosi, April 07.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’