Yanga imesimika mnara mwingine wa 5G uwanja wa Azam Complex baada ya kufumua Polisi Tanzania mabao 5-0 katika mchezo wa hatua ya 32 bora kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Lilikuwa suala la muda tu kwa mshambuliaji Joseph Guede ambapo leo amefungua rasmi akaunti yake ya mabao akiweka kambani mabao mawili yote yakitengenezwa na Augustine Okrah
Farid Mussa, Clement Mzize wakaongeza kabla ya Shekhan Khamis kufunga bao la tano kupitia mkwaju wa penati
Yanga imetinga hatua ya 16 bora kibabe ikiendeleza rekodi ya vipigo vya 5G
Sasa kituo kinachofuata ni CR Belouizdad siku ya Jumamosi mchezo wa ligi ya mabingwa utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE