Mchezo wa Jumamosi wa Jumamosi ligi ya mabingwa dhidi ya CR Belouizdad imetangazwa ni mtoko wa Pacome Day
Akizungumza kwenye Mkutano na Wanahabari, Meneja wa Habari na Mawasiliano Ali Kamwe amesema hii ni mechi muhimu ambayo mashabiki hawapaswi kubaki nyumbani
Kamwe amesema wapinzani wao CR Belouizdad watawasili nchini Jumatano, saa 3 kamili asubuhi, Februari 21, 2024
"Mechi hii tunakwenda na mtoko gani? Msimu huu katika mechi za nyumbani ligi ya mabingwa tulianza na mtoko wa Maxi, Stephane, Bacca Day na GSM Day"
"Sisi hatutaki unyonge, agenda yetu ni kumpiga mwarabu kwa Mkapa na pia kurejesha deni letu. Twendeni kwa Mkapa tukashangilie timu yetu. Tuhakikishe tunashangilia kwa dakika zote 90"
"Tunapaswa kuzungumza na wachezaji kwa muda wote ili kuwaweka katika presha kubwa wapinzani wetu kwa dakika zote 90"
"Hii ni mechi ambayo tunapaswa kwenda na hasira zote. Mashabiki ambao wako mikoani tunawaambia wajiandae na safari kuelekea mechi hii"
"Hii ni mechi ya maisha yetu, hatupaswi kupoteza hata alama moja. Ushindi unaanzia kwetu mashabiki, sisi tukiwa imani basi hata wachezaji wetu watakuwa na imani
"Hatujacheza kwa muda mrefu kwa Mkapa hivyo tunavyorudi ni lazima turudi na kishindi kikubwa"
"Jumamosi tumekubaliana itakuwa Pacome Day 'kitaalam zaidi'. Mtoko wetu uko hivi; Wananchi ambao mko tayari kupiga 'blich', pigeni'.Kama hutaki kupiga blich kichwani basi weka hata kwenye ndevu"
"Lakini pia unaruhusiwa kuchora au kupaka rangi iwe jina la Pacome, iwe namba ya jezi yake. Kutakuwa na zawadi kutoka GSM kwa mashabiki watakaopendeza zaidi kwenye Pacome Day," alisema Kamwe
Nae Mwenezi wa Yanga Jimmy Kindoki ametangaza kuanza kwa wiki ya hamasa kuelekea mchezo huo ambapo kesho Jumanne, timu ya hamasa itakuwa Mbagala Zakhiem kuanzia asubuhi mpaka jioni kuelekea mchezo wa kombe la FA dhidi ya Polisi Tanzania