Wiki ya kuelekea mchezo wa kuamua hatma ya Yanga katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika imeanza leo
Mapema klabu ya Yanga imetangaza viingilio kuelekea mchezo huo utakaopigwa Jumamosi, Februari 24 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 1 usiku
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kununua tiketi zao mapema lengo ni kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa
Kamwe amesema mechi hiyo ni kama fainali kwa Yanga, hawahitaji matokeo mengine tofauti na ushindi
Baadae leo, Yanga itazungumza na wanahabari kuweka mkakati kabambe kuelekea mchezo huo
Kiingilio cha chini Mzunguuko ni Tsh 5,000/- wakati VIP A ni Tsh 30,000/-, VIP B ni Tsh 20,000/- na VIP C ni Tsh 10,000/-
ADVERTISE HERE