Wakazi wa mkoa wa Morogoro na maeneo ya jirani, kesho Jumamosi watapata fursa ya kuwashuhudia mabingwa wa nchi Yanga wakichuana na KMC katika mchezo wa ligi kuu ya NBC ambao utapigwa uwanja wa Jamhuri
KMC ndio wenyeji wa mchezo huo na wameweka hadharani viingilio ambapo VIP ni Tsh 15,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-


Yanga tayari iko mkoani Morogoro ambapo leo itafanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Jamhuri
ADVERTISE HERE