Ni msimu wa rekodi kwa Yao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Feb 2024
Ni msimu wa rekodi kwa Yao

Yanga inaongoza mbio za ubingwa msimu huu ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kukusanya alama 40 katika mechi 15 ilizocheza

Miongoni mwa wachezaji wenye mchango mkubwa katika kikosi cha Yanga ni beki wake Muivory Coast, Kouassi Attohoula Yao (27)

Yao ,beki wa kulia ni kinara wa kutoa pasi za magoli 'asisti' akifanya hivyo mara sita sawa na winga wa Azam FC, Kipre Junior

Huenda msimu huu ukawa wa kifalme kwa Yao kutokana na rekodi za asisti zilivyo katika misimu mitatu iliyopita kwa wachezaji wanaocheza eneo la ulinzi

Katika misimu minne iliyopita kwenye Ligi Kuu Bara ni beki mmoja tu, Shomari Kapombe aliyeweza kutoa asisti kuanzia tatu na kuendelea kwenye kila msimu

Msimu uliopita Kapombe ndiye beki aliyetoa asisti nyingi zaidi akitoa assist nane, mpaka sasa Yao ana assist sita ikiwa ndio kwanza msimu uko nusu

Ukichukua asisti za Yao kwa msimu huu ukazipeleka msimu wa 2021/2022, basi angekuwa kinara wa kupiga pasi za mwisho katika msimu huo. 2021/2022 ulikuwa msimu mgumu kwa wakali wa Asisti kwani walioongoza walikuwa nazo sita pekee

Ni Abdulhaman Mussa wakati huo akiwa Ruvu Shooting na Reliants Lusajo aliyekuwa Namungo. Waliibuka vinara baada ya kila mmoja kupiga asisti sita. Kwa sasa wawili hao wote wako Mashujaa FC

Djuma Shaban ndiye aliongoza kwa mabeki waliotoa asisti nyingi msimu huo akitoa tano ambazo tayari Yao amezipita

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’