Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema anatarajia ushindani utakuwa mkubwa zaidi katika duru ya pili ligi kuu ya NBC hivyo lazima wajipange kukabiliana nao
Gamondi ameiongoza Yanga katika mechi 15 za duru ya kwanza, akiipeleka kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya ushindi kwenye mechi 13, sare moja na kupoteza mchezo mmoja
Gamondi amesema kuelekea duru ya pili, watahitaji kuwa bora zaidi ili kutimiza malengo yao ya kutetea ubingwa ligi
"Natarajia ugumu zaidi kwenye mechi za kumalizia ligi, nimewaambia wachezaji wangu hakuna timu inayokuja kwetu ikijiandaa kupoteza, tunaona jinsi mbinu za wapinzani zilivyo kwa sasa, unaona kabisa wanadhani tutashinda nyingi ndio maana huwa hawataki kucheza na kuamua kujilinda"
"Tunaheshimu mbinu zao lakini sisi lazima tuwe na njia tofauti ya kutafuta ushindi, tutakuwa na mabadiliko machache kulingana na aina ya wapinzani tutakaokutana nao, tunatakiwa kushinda kwa kiwango bora kila timu kwenye hizi mechi zitakazofuata itakuwa na hesabu zake ili ibaki salama," alisema Gamondi
Yanga inaanza mzunguuko wa pili kwa mchezo dhidi ya KMC ambao utapigwa Jumamosi, Februari 17 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro