Mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra amerejea na kujiunga na wenzake katika maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya KMC ambao utapigwa Februari 17
Diarra ni mchezaji wa mwisho kurejea kikosini baada ya kumalizika kwa michuano ya Afcon 2023 iliyofanyika Ivory Coast timu yake ya Taifa ya Mali ikitolewa hatua ya robo fainali
Diarra alidaka mechi zote za Mali katika michuano hiyo akiwa mmoja wa magolikipa waliong'ara
Haishangazi kuona tetesi kuhusu hatma yake n Yanga zilikuwa nyingi, habari njema kwa Wananchi ni kuwa mdaka mishale amerejea kuendelea na majukumu yake
ADVERTISE HERE