Juzi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons lilishudiwa tukio lisilo la kiungwana dhidi ya mlinzi wa kulia wa Yanga Yao Kouassi ambaye alikanyagwa na mchezaji wa Prisons Jeremiah Juma
Jeremiah alimkanyaga Yao mbele ya mwamuzi wa akiba lakini cha kushangaza hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa
Jambo jema ni kuwa tukio hilo lilinaswa na Camera za Azam TV, matarajio ya Wananchi ni kuona Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi ikichukua hatua stahiki dhidi ya Jeremiah
Ni tukio ambalo lingeweza kumsababishia Yao madhara makubwa. Mpira ni mchezo wa kiungwana matukio haya hayapaswi kufumbiwa macho
ADVERTISE HERE