The former speaker of Yanga Haji Manara has given free advice to striker Fiston Mayele to stop arguing on the internet because he cannot win the battle
Manara has said that no Yanga fan can attack Mayele on the internet because it was the Yanga people who made him famous and fought for him in difficult times
Through the pages of his Instagram network, yesterday Mayele dropped suspicions that there are fans of Yanga who have hatred towards him while accusing us of being subjected to superstitious events (being thrown into the water)
Through his social media page, Manara has advised Mayele to stop fighting with fans online
"Rafiki yangu Fiston, kila jina zuri Wanayanga tumekupa, kila heshma uliyostahili kwa kile ulichofanya kwetu tumekuonyesha,Tulikwita Mfalme na mimi nikawa natanguliza jina la king Pele kabla ya utajo wako, Tulikuimba kwa kila nyimbo yenye hadhi, ukawa ukienda hata kanisani Jumapili unakaa viti vya mbele,hata kwenye Profile yako ya Insta umeandika ni Top Scorer wa CC Cup 2023, ni connection direct na @yangasc hiyo!
Ulipodhihakiwa na Wapinzani wetu na baadhi ya Wachambuzi, Wanayanga ndio waliosimama na ww, unakumbuka ile vita ya top scorer na George Mpole? Huna kumbukumbu nzuri na Wananchi hata ktk hili? Alichangiwa hadi michango lakini tulisimama na ww!! Ulipokuwa hufungi ulinangwa mno lakini Wanayanga waliendelea kukutia nguvu na kukupa ujasiri,Uliandikiwa Makala nyingi na baadhi ya Wachambuzi wanaokuchuuza leo, tukatoka hadharani kukutetea bila haya,mm binafsi ndio binadaamu niliekupost mara nyingi zaidi ktk miaka hii kuliko yoyote yule, Mshindani wako may be ni @zaiylissa
Inawezekana Wachache miongoni mwetu wanakosea lakini kuitaja @yangasc na Tanzania yetu ktk andiko lako sio sawa,ni Wananchi waliokuwa wakibezwa zaidi kwa ww kutopata muda mwingi wa kucheza kule Afcon, lakini bado unaona watu wa Yanga ndio wabaya wako!!
Mm Nakupenda mno na ww na Nchi hii inajua, lakini acha nitumie platform ile ile uliyotumia ww kukuasa kitu, huku mitandaoni huwezi kupendwa na kila Mtu hata uwe Messi au Ronaldo,hii ni dunia nyingine kabisa na inajitegemea na kama unaendelea kutumia Social Media tambua hilo na huna budi kukubali,ikiwa Rais wa Nchi anabezwa mitandaoni itakuwa ww? Mwenzio napost hadi Ijumaa Kareem anatokea Mtu anakutusi bila sababu.
By the way hata ww ulitucharura baada ya mechi yenu na Morocco,iweje ukasirike ukiguswa kidogo? Vumilia na hizo ndio raha na karaha za Instagram,usiingizwe mkenge na Watu ambao wanawaita Washabiki wetu Washamba ilhali wao kutwa kuwabeza Wachezaji wao hadharani, halaf wasichokijua, bora ushamba kuliko undigili.
Nimalizie kwa kukwambia,Yanga SC hatuna kinyongo na ww na tunathamini sana mchango wako kwetu ,na still tunakuombea kheri nyingi huko ulipo,kiufupi ww bado ni Shujaa kwetu na alama yako haitafutika pale Jangwani"
Tangu alipoondoka Yanga, Mayele amekuwa na wakati mgumu wa kuendeleza kasi yake ya kuzifumania nyavu akiwa na klabu ya Pyramids na hata timu ya Taifa