Jana Yanga ilifunga mzunguuko wa kwanza ligi kuu ya NBC kibabe kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya
Mabingwa hao watetezi wamemaliza mechi za duru ya kwanza wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na alama 40. Ni alama tano tu zilizodondoka katika duru ya kwanza
Mchezo wa kwanza wa duru ya pili ni dhidi ya KMC ukitarajiwa kupigwa Alhamisi Februari 15 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro
KMC wameomba kutumia uwanja wa Jamhuri kuwa uwanja wao wa nyumbani kufuatia uwanja wa Uhuru kufungwa kwa ajili ya ukarabati
KMC 'wamekimbia' Azam Complex kwani wanakumbuka kilichowakumba katika uwanja huo kwenye duru ya kwanza!
ADVERTISE HERE