Ivory Coast wabakisha taji la Afcon nyumbani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Feb 2024
Ivory Coast wabakisha taji la Afcon nyumbani

Usiku wa kuamkia leo, Sebastien Haller alikuwa shujaa wa Ivory Coast  wakati The Elephants walipotoka nyuma na kuwashinda Nigeria mabao 2-1 na kushinda fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 wakiwa nyumbani

Mshambulizi huyo, ambaye pia alifunga bao la ushindi wa nusu fainali, aliunganisha krosi ya Simon Adingra zikiwa zimesalia dakika tisa kukamilisha mchezo huo kipindi cha pili na kuibua shangwe kali jijini Abidjan

William Troost-Ekong alikuwa ameiweka Nigeria mbele dakika saba kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza wakati beki huyo wa kati aliporuka juu zaidi na kufunga kwa kichwa

Franck Kessie alifunga bao la kusawazisha dakika ya 62 kutokana na kona ya Adingra ambaye alitajwa kuwa mchezaji bora chipukizi wa michuano hiyo

Ivory Coast haikuwa na mwanzo mzuri katika michuano hiyo ikipenya hatua ya 16 kupitia 'best looser' lakini baadae kila kitu kikabadilika hadi kuwa mabingwa

Ivory Coast walinyakua taji la tatu la fcon na ushindi waliosatahili kuupata dhidi ya Nigeria

Tanzania ilishiriki michuano hiyo kwa mara ya tatu lakini ilitolewa hatua ya makundi baada ya kupoteza mchezo mmoja na kutoka sare michezo miwili

Michuano hiyo inatarajiwa kufanyika tena mwakani (2025) nchini Morocco na 2027 itafanyika katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’