Kikosi cha Yanga kiko mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo wa kwanza wa mtoano kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Welayta Dicha ya Ethiopia.
Mchezo huo utapigwa siku ya Jumamosi, April 07 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mazoezi ya Yanga yanayofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri yanasimamiwa kikamilifu na kocha Mkuu wa timu hiyo George Lwandamina.
Lwandamina amepania kuipeleka Yanga hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.
Mwaka 2016 Yanga wakati huo ikinolewa na Hans van pluijm kocha wa sasa wa Singida United ilitinga hatua ya makundi ya kichuano hiyo ambayo hata hivyo haikufanya vizuri.
Kwenye mahojiano yake na moja ya mtandao maarufu wa michezo, Lwandamina amesema anafurahishwa na ari ya wachezaji wake kuelekea mchezo huo.
Amesema wachezaji wote wa kikosi cha Yanga wamekuwa wakifanya mazoezi kwa nguvu kila mmoja akielekeza fikra zake kuikabilia Welayta Dicha.
"Maandalizi yanaendelea vizuri. Wachezaji wote wameelekeza fikra zao vizuri kabisa kwenye mchezo na kikubwa tunaendelea kufanyia kazi mapungufu ambayo yamekuwa yakijitokeza kwenye mechi zilizopita,"amesema Lwandamina.
Kikosi cha Yanga kinatarajia kurejea jijini Dar es salaam kesho Alhamisi kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo huo.
Wapinzani wao wanatarajia kuwasili leo Jumatano mchana.

ADVERTISE HERE