Wakati Azam Fc na Simba zikuchuana leo katika mchezo wa ligi kuu unaopigwa CCM Kirumba, Wananchi watakuwa paleeeeee kileleni wakishudia ugomvi wa ndugu
Mmiliki wa Azam Fc anafahamika ni Mwanachama na amewahi kuwa kiongozi wa Simba hivyo ni sahihi kusema ni ugomvi wa ndugu!
Matokeo yoyote ya mchezo huo hayataiathiri Yanga kwa kuwa hakuna timu inaweza kufikia pointi ambazo Yanga amekusanya (37)
Kama timu hizo zitatoka sare itakuwa faida zaidi kwa Yanga kwani gap litaongezeka kwa wote wawili lakini kama timu moja itafungwa, gap litaongezeka kwa upande wa timu hiyo
Jambo la uhakika ni kuwa Wananchi wataendelea kubaki kileleni baada ya dakika 90 za mchezo huo

Mchezo unaofuata kwa Yanga ni dhidi ya Tanzania Prisons ukitarajiwa kupigwa Jumapili, Februari 11 katika uwanja wa Sokoine