Leo Yanga inashuka uwanja wa Azam Complex kuikabili Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Wananchi wataendelea kukosa huduma ya wachezaji wao muhimu mlinda lango Djigui Diarra na kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki
Hata hivo habari njema ni kuwa wachezaji hao watawasili nchini kabla ya mchezo dhidi ya Mashujaa Fc utakaopigwa Februari 08 dimba la Azam Complex
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wachezaji hao wamechelewa kurejea nchini kwa sababu timu zao za Taifa zilicheza hatua ya mtoano Afcon 2023
Burkina Faso anayoitumikia Aziz Ki iliondoshwa na Mali hatua ya 16 bora Januari 30 wakati Mali anayocheza Diarra iliondoshwa na Ivory Coast hatua ya robo fainali Februari 03
Aidha Kamwe amethibitisha kuwa kiungo Mudathir Yahya ambaye alikosa mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar, amerejea kikosini tayari kuikabili Dodoma Jiji