Tunawasubiri Singida United uwanja wa Taifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Apr 2018
Tunawasubiri Singida United uwanja wa Taifa
Baada ya mchezo dhidi ya Welayta Dicha April 07, Yanga itashuka tena kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Singida United kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 22 Jumatano ya April 11.

Mchezo huo utakuwa na umuhimu wa kipekee kwa Yanga.

Kwanza ni wa kulipa kisasi cha kuondoshwa na timu hiyo kwenye michuano ya kombe la FA, pili ni kupata ushindi utakaoiweka Yanga karibu na mahasimu wao Simba katika mbio za ubingwa.

Ushindi wa mabao 2-0 iliyopata Simba dhidi ya Njombe Mji leo, umeifanya ifikishe alama 49, alama tatu zaidi ya Yanga iliyo nafasi ya pili.

Simba inatarajiwa kushuka dimbani April 09 kuikabili Mtibwa Sugar na Yanga kucheza na Singida United siku mbili baadae.

Ni muhimu kwa Yanga kuendelea kuibana mbavu Simba kabla timu hizo hazijakutana kwenye mchezo wa kukata na shoka April 29.

Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina ambaye kikosi chake kimeweka kambi mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo dhidi ya Welayta Dicha, anawaandaa wachezaji wake kikamilifu kwa ajili ya michezo yote miwili.

Baada ya kucheza na Welayta Dicha April 07, Yanga itakuwa na siku tatu za kujiandaa kabla ya kuivaa Singida United.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’