Kikosi cha Yanga kimesafiri mapema leo kuelekea Bukoba kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa uwanja wa Kaitaba Ijumaa, Februari 02 2024
Katika kikosi cha wachezaji 20 waliosafiri, walinzi Ibrahim Bacca na nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto wamebaki jijini Dar es salaam
Wachezaji hao ambao wamerejea hivi karibuni kutoka Ivory Coast baada ya kushiriki michuano ya Afcon 2023, walipata majeraha katika michuano hiyo
Aidha Dickson Job amejumuishwa katika kikosi hicho na bila shaka ataongoza safu ya ulinzi sambamba na Gift Fred

Habari njema kwa Yanga pia ni urejeo wa kiungo Khalid Aucho aliyemaliza adhabu ya kufungiwa mechi tatu
Aucho alikosa mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Tabora United na Housung Fc
Ushindi katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar, utairejesha Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi