Yanga imefuzu raundi ya tatu ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Housung Fc ya Njombe
Clement Mzize ameanza vyema michuano hiyo kama alivyofanya msimu uliopita akifunga hat-trik
Mabao mengine ya Yanga yalifungwa Jonas Mkude ambaye alifungua kalamu ya magoli, Skudu akaongeza la pili kabla ya Mzize kufunga mabao yake matatu
Wakati wa mapumziko Yanga ilimtambulisha mshambuliaji Joseph Guede aliyesajiliwa kwenyee dirisha dogo
ADVERTISE HERE