Taifa Stars leo itaumana na DR Congo katika mchezo muhimu wa kuwania kutinga hatua ya mtoano michuano ya Afcon 2023 inayoendelea huko Ivory Coast
Pengine leo itashuhudiwa 'battle' ya aina yake kati ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga Fiston Mayele anayeitumikia DR Congo dhidi ya safu ya ulinzi ya Stars ambao inatarajiwa kuongozwa na beki kisiki Ibrahim Bacca na Bakari Mwamnyeto au Dickson Job
Kocha wa DR Congo Sebastien Desabre leo anaweza kumuanzisha Mayele katika kikosi chake akiamini yeye anawafahamu vyema walinzi wa Stars aliocheza nao Yanga kwa misimu miwili

Hata hivyo Mayele nae atakuwa na kazi ngumu mbele ya Bacca na wenzake kwa kuwa hata wao wanafahamu ubora na madhaifu yake
Hii itakuwa mechi ya kwanza Mayele anacheza dhidi ya Tanzania tangu alipoondoka Yanga kujiunga na Pyramids msimu uliopita